Karibu! Tafadhali soma ujumbe ufuatao kabala hujaanza kujibu maswali: 

Fomu ya Ridhaa ya kushiriki kwenye “Usaidizi wa Serikali kwa Wakimbizi  Kujenga Makazi Mapya, Muunganiko wa Kijamii na Matokeo ya Ajira katika BC: Tafakari ya Muongo wa Kuwaslili ili kupanga kwa ajili ya idadi ya watu ijayo” 

Mtafiti Mkuu: Dr. Daniel Hiebert, , Idara ya Jiografia, Chuo kikuu cha British Columbia 
1984 West Mall, Vancouver, BC Canada V6T 1Z2  |  dan.hiebert@ubc.ca 
Mtafiti Msaidizi: Grace Newton, Idara ya Jiografia, Chuo kikuu cha British Columbia 
1984 West Mall, Vancouver, BC Canada V6T 1Z2  |  grace.newton@alumni.ubc.ca 

Mfadhili: Utafiti huu unafadhiliwa kwa msaada kutoka Uhamiaji, Wakimbizi na Uraia Canada. 

Kusudi: Mradi huu utatusaidia kuelewa vema uzoefu wa jinsi serikali inavyosaidia kuunganisha wakimbizi na jamii katika jimbo la Britisha Columbia katika miaka kumi iliyopita. Tutachunguza jinsi wakimbizi wanavyotumia huduma za jamii humu BC, na tutachanganua kama huduma hizi zinasaidia. Vile vile tutajadili jinsi wakimbizi wanavyoelewa muunganisho na mafanikio, na tutatambua vikwazo vya mafanikio ya kuuganisha. Habari hizi itaturuhusu kuelewa jinsi mabadiliko ya sharia ya wakimbizi ya serikali ya shirikisho ilivyohusiana na muunganisho na itatupa fursa ya kutoa mapendekezo jinsi ya kuwezesha muunganisho wa wakimbizi katika British Columbia. 

Utaratibu wa Uchunguzi: Utajaza fomu ya maswali kwenye mtandao kuhusiana na uzoefu wako wa kujenga makao mpaya Canada. Fomu ya maswali itachukua takribani dakika 10-15, utaulizwa kuhusu maisha yako ya kila siku, pamoja na kazi, elimu, na makazi. Kujibu maswali yote ni chaguo la hiari, na uko huru kujiondoa na kusimamisha ushirikaji wako mudo wowote. 

Matokeo ya Mradi: Matokeo yatasambazwa kama ukurasa mmoja katika lugha mbali mbali, Makala kwenye majarida yaliyopitiwa na wataalamu, mikutano ya kwenye mitandao, Wakimbizi na Uraia ya Canada.  

Faida zinazowezekana: Hakuna faida za wazi kwako katika ushirikaji wako katika uchunguzi huu. Lakini, uchunguzi utakupatia fursa ya kushirikiana na wengine ukiwa kama mkimbizi uliyesaidiwa na serikali ulipokuja Canada. Uelewo wako utatumika kuboresha mazoefu ya kuanzisha makazi mapya huko mbeleni. 

Hatari Zinazoweza kujitokeza: Maswali ya uchunguzi kimsingi yanahusu maisha ya kila siku, na hatutegemei kwamba maswali yatapelekea kukuudhi. Lakini, uko huru kusitisha ushirikaji wako muda wowote na kwa sababu yoyote ile. Hupaswi  kushirikiana na mtu mwingine kuhusu sababu hiyo. Kama uchunguzi huu utaleta hisia zitakazo hitaji msaada wa kuzikabili, nyenzo zitaambatanishwa mwanzoni  mwa uchunguzi.

Usiri: Hatutakuuliza jina lako au anwani kama sehemu ya uchunguzi huu. Data za utafiti zitatunzwa katika mafaili ya komputa yakihifadhiwa kwenye USB inayolindwa na nenosiri. Hii itatunzwa kwenye mtoto wa meza unaofungwa wakati haitumiki. Mwishoni mwa utafiti huu, fomu zozote zitawekwa katika bahasha iliyofungwa katika kabati na kuchanwa-chanwa baada ya miaka mitano.

Mhamasisho/ Fidia: Hutafidiwa kipesa kwa kushiriki  kikamilifu katika utafiti huu.

Mawasliano kwa maelezo zaidi kuhusu utafiti huu: Kama una swali lolote au unahitaji maelezo zaidi kuhusu utafiti huu,wasiliana na Dr. Daniel Hiebert (dan.hiebert@ubc.ca) au Grace Newton (grace.newton@alumni.ubc.ca)

Mawasiliano kw ajili ya wasiwasi au malalamiko kuhusu utafiti huu: Kama unao wasiwasi au malalamiko kuhu haki zako kama mtafiti mshiriki na /au uzoefu wako kutokana na kushiriki katika utafiti huu, wasiliana kwa simu na Ofisi ya Maadili ya Utafiti ya UBC kwa namba 604-822-8598 au kama masafa ya mbali barua pepe RSIL@ors.ubc.ca au simu isiyo ya malipo 1-877-822-8598. 

Ridhaa: Ushirikishwaji wako katiki utafiti huu ni wa kujitolea na unaweza kukataa au kujitoa kwenye utafiti muda wowote. Kwa kubonyeza “anza uchunguzi” unaashiria ridhaa yako ya kushiriki katika utafiti huu.

Kama una umri wa miaka 14-17, tafadhali hakikisha mzazi au mlezi anasoma ujumbe hapo juu. Na pia asome ujumbe hapa chini.

Fomu ya kuafiki – Utafiti was usaidizi wa Serikali kwa Wakimbizi.

Kichwa cha Mradi wa Utafiti: “Makazi ya Wakimbizi  wanaosaidiwa na  Serikali, Kujumuisha kijamii na matokeo ya nafasi za kazi katika BC: Kutafakari uwasili wa mwongo mmoja ili kupanga kwa ajili ya idadi ya watu ijayo”   

Nani anasimamia utafiti? Dr.Daniel Hiebert, profesa katika idaraya Jiografia katika chuo kikuu cha British Columbia ni msimamizi wa utafiti. Grace Newton, mwanafunzi wa shahada ya juu latika idara ya Jiografia ya Chuo Kikuu cha British Columbia,  anasaidia kama mtafiti msaidizi. Uhamiaji, Wakimbizi and Uraia ya

Canada inafadhili utafiti wetu. Kama nina swali lolote kuhusu utafiti huu, naweza kuwasiliana na Dr. Hiebert kupitia dan.hiebert@ubc.ca na Grace Newton kupitia grace.newton@alumni.ubc.ca.

Mwaliko: Ninaalikwa kushiriki kwenye utafiti huu kwa sababu nilikuwa mkimbizi aliyesaidiwa na serikali ya Canada. Kurasa zifuatazo zinaeleza utafiti ili niweze kuamua kama nitashiriki au hapana. Ni juu yangu kama nataka kuwa kwenye utafiti huu. Hakuna yoyote atakayenishinikiza kuwa sehemu ya utafiti na hakuna yeyote atakayenikasirikia endapo sitakuwa sehemu ya utafiti huu.

Ninapaswa kuwa kwenye utafiti huu? Siyo lazima nishiriki kwenye utafiti huu kama sipendi kufanya hivyo. Iwapo nitachagua kushiriki ninaweza kusitisha ushirikaji muda wowote.  Kama ninataka kushiriki katika utafiti huu, nitatakiwa kusaini fomu hii. Wazazi/walezi wangu watatakiwa kusaini fomu ya idhini kabla sijajiandikisha kwenye utafiti huu; lakini siyo lazima nishiriki hata kama watasaini fomu ya idhini. Nitachukua muda kusoma maelekezo yafuatayo kwa uangalifu na kujadili na familia yangu kabla ya kuamua. Nafahamu kuwa ninapaswa kujisikia huru kuzungumza na Dr. Hiebert au Grace Newton kama kuna jambo ambalo halipo wazi hapa chini. Naweza kuchagua kuwa kwenye utafiti, kutokuwa kwenye utafiti, au kuchukua muda kabla ya kuamua. Hata kama niatamua kwa sasa kuwa sehemu ya utafiti, naweza kubadili mawazo yangu hapo baadaye, na siyo mpaka nitoe maelezo yoyote ya kwa nini naondoka kwenye utafiti. Naweza kuwauliza watafiti swali lolote nitakalokuwa nalo wakati wowote katika kipindi nitakapokuwa nashiriki kwenye utafiti. 

Kwanini tunafanya utafiti huu? Watafiti wanafanya uchunguzi huu ili kuelewa jinsi ambavyo usaidizi wa wakimbizi na serikali unavyowajengea maisha humu British Columbia. Mchakato huu mara nyingi unajulikana kama muunganishwo, na unajumuisha mambo kama vile kupatiwa kazi, kutafuta sehemu ya kuishi, na kujenga marafiki. Utafiti huu utaniuliza kuhusu maisha yangu ya kila siku tangu nimewasili Canada na utaniwezesha kushirikiana na wengine katika kueleza mawazo yangu juu ya yapi yangenisaidia mara tu nilipofika. Watafiti watatumia majibu yangu kuelewa mazingira ya kuwa mkimbizi msaidiwa na serikali wa zamani katika nchi ya Canada. Utafiti utajumulishwa katika tasninifu ya shahada ya pili ya Grace Newton pamoja na ripoti kwenda Uhamiaji, Wakimbizi na Uraia Canada.

Nini kitanitokea kwenye utafiti huu? Kama nitachagua kushiriki katika utafiti huu, nitaulizwa baadhi ya maswali kuhusiana na maisha yangu ya kila siku, pamoja na shule, nyumbani, na maisha ya familia. Maswali yatachukua dakika 10-15.

Kunaweza kutokea kitu chochote kibaya? Siyo rahisi kuwa kitu chochote kibaya kinaweza kutokea kwangu katika kushiriki kwenye utafiti huu. Lakini, kama kuna swali lolote litakaloniletea hisia za huzuni, au wasiwasi, nitaongozwa kwenye nyenzo za kunisaidia kupambana na hisia hizi. Nitaweza kujitoa wakati wowote, na hakuna atakayenikasirkia iwapo sitapenda kundelea kushiriki.

Kuwa katika utafiti kunaweza kunisaidiaje binafsi? Ukamilishaji wa utafiti hautanisaidia mimi moja kwa moja. Lakini, watafiti watatumia habari zangu ili kuelewa mazingira ya kuwa mkimbizi msaidiwa na serikali wa zamani katika nchi ya Canada.

Nani atafahamu kuwa niko kwenye utafiti? Mimi pekee, wazazi wangu, na watafiti watafahamu kuwa niko kwenye utafiti. Itakapofika wakati wa kutangaza utafiti, watafiti hawatajumuisha jina langu au habari zingine zitakazopelekea wengine kufahamu kuwa nilishiriki kwenye utafiti.

Nani wa kuwasiliana naye kama nina maswali kuhusu utafiti? Kama una maswali au mahitaji ya kupata habari zaidi kuhusu huu utafiti kabla au wakati wa ushiriki, naweza kuwasiliana na Dr. Hiebert (dan.hiebert@ubc.ca) au Grace Newton (grace.newton@alumni.ubc.ca).

Nani wa kuwasiliana naye kama nina wasiwasi au malalamiko kuhusu utafiti? Kama nina wasiwasi au malalmiko kuhusu haki zangu kama mwanautafiti mshiriki na/au uzoefu wangu kutokana na kushiriki katika huu utafiti, Nitawasiliana kwa simu na Malalamiko ya Watafiti Washiriki ndani ya ofisi Maadili ya Utafiti ya UBC kwa namba 604-822-8598.

Kubonyeza kibonyezo  'inayofuata' ina maana:

• Nimesoma na kuelewa fomu hii  ya kuafiki kwa kijana.

• Nilikuwa na muda wa kutosha kufikiria habari iliyotolewa na kulizia ushauri kama ni muhimu 

• Nilikuwa na nafasi ya kuuliza maswali na kupata majibu yanayokubaliwa kwa maswali yangu

•  Ninaelewa kuwa habari zote zilizokusanywa zitawekwa kwa usiri

• Naelewa kuwa ushiriki wangu katika utafiti huu ni wa kujitolea na kuwa niko huru kabisa kukataa kushiriki au kujitoa kwenye utafiti muda wo wote.

• Naelewa kuwa naweza kuendelea kuuliza maswali, wakati wowote, kuhusiana na ushirikishwaji wangu katika utafiti.

• Naelewa kuwa kama nikiweka jina langu mwishoni mwa fomu hii, ina maana nakubali kuwa kwenye utafiti huu.

Nakubali kushiriki katika utafiti huu.

There are 69 questions in this survey.

A note on privacy
This survey is anonymous.
The record of your survey responses does not contain any identifying information about you, unless a specific survey question explicitly asked for it. If you used an identifying token to access this survey, please rest assured that this token will not be stored together with your responses. It is managed in a separate database and will only be updated to indicate whether you did (or did not) complete this survey. There is no way of matching identification tokens with survey responses.